CHUO CHA KATEKESI EMMAUS
Shirika liliendeleza Malezi ya misingi ya kitawa kwa masista kwa kuwapeleka shule na Vyuo ili kujiendeleza Kiakili na Kiroho hususani Chuo cha Kichungaji cha Teolojia huko Rauya Moshi, kinachosimamiwa na kuendendeshwa na Masista wa Kazi ya Roho Mtakatifu.Jubilee hii tunamshukuru Mungu sana kwa ajili ya Masista wa Kazi ya Roho Mtakatifu Rauya kwa kuwa Sehemu Endelevu kwa utume huu wa Katekesi tunaoutoa katika Kanisa. Kwa namna ya pekee tunamkumbuka hayati Padre Fridolin Portman aliyekuwa Mtaalamu wa Historia ya Kanisa na mkufunzi wa mambo ya Katekesi huko Mnero- Ndanda na Galapo- Mbulu. Kutokana na ari yake ya kuwaunda Makatekista waweze kueneze Habari Njema katika kanisa la leo,wenye kujua kusoma alama za nyakati mawazo yake yalichipua uhitaji wa Chuo cha katekesi ndani ya shirika letu, ili kuwaelimisha walimu wa dini katika Parokia, Vagango, Shule na Vyuo katika kanisa katoliki ,ili kuitikia Agizo la Yesu kutangaza Injili kwa Mataifa (Lk.24: 47).Baada ya kumshirikisha Mhashamu baba askofu Amedeus Msarikie na kukubali na kuweka Baraka zake. Ujenzi ulianza rasmi mwaka 1990 na tarehe 25/9/1993 Mhashamu baba askofu Amedeus Msarikie alibariki rasmi Kanisa na Majengo.
ENEO KILIPO CHUO NA JINA EMMAUS
Pia Jubilei hii ya Chuo cha Katekesi tulimo tunamkumbuka kwa shukrani kubwa hayati baba Joseph Kamili Kanje na Familia yake nzima kwa maongozi ya Mungu kutukaribisha sisi Masista Wakapuchin wa Maua kutumegea Eneo la shamba lao ili kwa uwepo wetu kuleta Mwanga wa Injili.
Kutafakari lengo la Utume wetu wa katekesi Jina “Emmaus” ni jina la Ubatizo kwa eneo hili – Hasa kuhusisha na kujihidhirisha kwa Yesu Kristo Mfufuka kwa wafuasi wawili wa Emau. Wafuasi waligubikwa na giza la huzuni baada ya mateso na Kifo cha Bwana wao Yesu waliyemtumainia. Baada ya kujidhirisha kwao kwa kumega mkate, giza liliondolewa na wakamtambua, mioyo yao iliwaka na kurudi Yerusalemu na kuwapasha habari ya Ufufuko kwa ndugu zao. Tafakari hiyo ikawa ni hamu yetu kwamba Kila ajaye Emmaus akutane na Yesu Kristo Mfufuka na ari kubwa AKATANGAZE INJILI KWA NDUGU ZAKE.
Tarehe 25/ 1/ 1994 chini ya uongozi wa Mhudumu mkuu Mama Immaculata Haas wa Masista Wakapuchin wa Maua, Walitumwa rasmi Masista watatu kuja hapa Emmaus Sanya –Juu ambao ni Sr. Asintha Inyasi Massawe,Calista Mtenga na Apolina Masenge. Wakaanza kustawisha mahali hapa na kuanzisha Utume wa Katekesi. MAFUNZO YA KATEKESI
Mwaka 1994 hadi 1995 Kituo cha Emmaus Sanya -Juu kilikuwa na utaratibu pamoja na mipango thabiti; kwa makundi yote ya Karismatiki katoliki pamoja na semina na mafungo.Hatimaye chuo kilianza kutoa mafunzo kwa miezi mitatu mitatu. Baada ya mang`amuzi ya mwaka mmoja kozi ya miaka miwili ilianzishwa rasmi mwaka 1995. Mwaka 1996 wahitimu wa kwanza walipewa Vyeti. Wengi waliokwisha kupata elimu hii wanaendelea kufanya utume wao katika majimbo mbali mbali ndani ya nchi na hata nje ya Tanzania. KOZI YA MIAKA MIWILI
Kwa mangàmuzi na ushirikiano wa Idara ya Katekesi TEC ilionekana ni vyema kuendesha kozi ya Ukatekekista kwa miaka miwili ili kumwezesha Katekista kupata kwa kina zaidi kinadharia na vitendo ili kuwa na uelewa mpana katika kuishi Imani yake na kuishuhudia kwa wengine. Mwaka 1997 hadi leo tunapoadhimisha Jubilee hii kozi ya ukatekista hapa Emmaus Sanya – Juu inaendeshwa kwa miaka miwili na kuwapokea wanachuo. Makatekista na mafunzo hutolewa Kimzunguko yaani wanafunzi wa mwaka wa kwanza na pili wanasoma pamoja, Mwanachuo wa mwaka wa pili humaliza, na hufanya Mitihani ya TEC na Wahitimu hutumwa rasmi na Baba askofu kupewa Vyeti vya Chuo na TEC. Kutokana na Neema za Mungu mwenyewe na Utendaji wake kupitia ndugu wengi waliochangia Vipaji vyao na Karama zao katika kuwaunda Makatekista ambao ni wengi idadi yao.Tangu chuo kianzishwe rasmi miaka 25 iliyopita kimetoa Makatekista wapatao 546 toka majimbo mbalimbali katika kanisa kanisa la Tanzania na pia mashirika ya watawa wa kiume na kike.Hatuwezi kutaja majina mmoja mmoja tunatambua majimbo: Jimbo Katoliki Moshi, Same, Mbulu, Morogoro, Ifakara, Ndanda, Shinyanga, Kahama, Iringa, Njombe, Tanga, Singida, Sumbawanga, Majimbo makuu Katoliki Arusha, Dar-es-Salaam, Dodoma, Tabora MASHIRIKA YA KITAWA
Shirika la Passionist Frs Ndugu Wakapuchin, Wabenedictine wa Ndanda na Sumbawanga Masista wa CDNK Huruma, Gemma na Misericordian Dodoma, Charles Borromeo Kia, Moyo Safi wa B.K. Maria Musoma, Wafransisko wa Bwana Arusha,Rosmiania Srs Tanga, Masista wa Huruma ya Mungu – Tanga , WasistaWafransisko wa Kristo Mbulu, Mchungaji Mwema Same, Shirika la PUMA – Singida. Shirika La Grail – Same, Shirika la Mama wa Mkombozi Mbulu, Shirika Maria Mkingiwa Dhambi ya asili – Dar-es-Salaam, Masista Wakapuchin Maua, Masista wa Agustinian Arusha.Tunawashukuru wote waliowatuma Makatekista wao kupata Elimu hii ya Katekesi wawe “ Chumvi na Taa kwa ulimwengu,” (Mt. 5: 13-14) Wengi wao ni Walezi katika Mashirika yao, Wakurugenzi wa katekesi majimboni, Wakuu wa Mashirika, Wakuu wa Vyuo na pia Kufanya kazi katika Vyombo vya habari mf.Radio Maria UONGOZI CHUO NA WAKUFUNZI
Kuja kwao na Mafanikio yao yangekuwa bure kama kusingekuwa na Uongozi na wakufunzi wenye Weledi katika Taaluma ya Katekesi.Hivyo kwa shukrani kubwa kwa Mungu tunawatambua na kuwataja hapa Waalimu walioitikia Wito wa Yesu kushiriki kazi yake ya Ualimu na malezi katika kipindi hiki cha miaka 25. Tunamkumbuka Mhashamu baba askofu Amedeus Msarikie kwa himizo na ukubalio wake kama mkuu wa Jimbo na utayari wake kuwatuma Mapadre kuja kufundisha Makatekista. PiaMhashamu baba askofu Isaac Amani ambapo ni askofu Mkuu Jimbo kuu Katoliki Arusha alihimiza kwa dhati Umuhimu na Utume wa Makatekista katika Kanisa.Tunamshukuru Mhashamu baba askofu Ludovic Joseph Minde wa jimbo letu la Moshi kuvaa viatu hivyo hivyo katekesi ikolezwe.
Tunamkumbuka baba askofu mstaafu Josephat Louis Lebulu wa Jimbo kuu katolikiArusha, kwa kuhimza Malezi, kutushauri na pia kutuma waalimu kufundisha Makatekista. Pia tunamkumbuka baba askofu mstaafu Telesephor Mkude wa Morogoro aliyeshirikiana nasi alipokuwa Idara ya katekesi TEC, na kushiriki nasi mahafali mwaka 2005 na aliyekuwa Mkurugenzi Sr.Claudia Mashambo. Wakati wake uliandaliwa rasmi Muhutasari wa vyuo vya Katekesi wenye masomo 15 ambao unatumika mpaka sasa na umetumika takribani miaka 40. WAALIMU.
Sr. Asinta Massawe alikuwa mkuu wa kwanza wa chuo chetu kuanzia mwaka 1995 hadi 1999 kwa sasa ni marehemu apumzike kwa amani,wakisaidiana na Sr. Apolina Masenge na Sr. Calista Mtenga .Hawa kwa jitihada zao na wakuu wa shirika kwa nyakati mbali mbali walipokea makatekista walei, walelewa na Masista wa Mashirika mbalimbali kati yao wamekuwa masista na mmoja ni Padre Erasto Ngwabali Shirika la Passionist. Mwaka 2000 hadi 2009 aliyeongoza Chuo ni Sr. Apolina Masenge na Sr. Calista mtenga alikaimu uongozi wa chuo kwa miezi tisa. Sr. Pauline Urio aliongoza tangu mwaka 2009 hadi Mwaka 2019, Mwaka 2020 hadi 2021 ni Sr. Juliana Gurty na kuanzia mwaka 2021 hadi sasa ni Sr. Pauline Urio. Kwa bidii na ushujaa wao walishirikiana sana na wahashamu mababa askofu wa jimbo katoliki Moshi. Tunawashukuru sana hawa Masista kwa kazi zao nzuri walizofanya hapa Chuoni. Pamoja na walioshiriki katika huduma hii ya ufundishaji Masista Wakapuchin wa Maua.Sr.Kristiana Njau, Sr. Scholastica Sulle, hayati Sr. Anastazia Mwanga, Sr. Adela Massawe, Sr.Ponsiana Massawe, Sr. Romana Mtenga. Pia tunamkumbuka katekista Hugolino Edward Marrow aliyefundisha miaka 10 na kuwa Karani katika kipindi hiki chote. Pia Idara ya Kichungaji na Idara ya Katekesi Jimbo kwa ushirkiano wao wengine wao walishaitwa na Mungu Pd. Agustine Mringi na Pd. Evarist Laswai: Tunawakumbuka Pd. Gebra Kimaro, Pd. Mark Begaya, Pd.Apolinari Kiondo, Pd. Apolinari Ngao, Pd. Landeline Makiluli, Leon Monoruwa, Pd. Leodegard Massawe, Pd. Evarist Ngawiliau, Pd.Severian Mafikiri,Pd. Daniel Amani. Chuo Chetu kipo katika Parokia ya Utatu Mtakatifu Sanya –Juu, pia Parokia jirani Naibili,Kigango cha Donyomurwak. Tunashukuru Makatekista waliweza kufanya Mazoezi ndani yake. Tunataja Maparoko : Pd. Ambrosi Mosha,Pd. Stanslaus Salla, Apolinari Kiondo, Deogratias Matiika, Pd. Riziki Kimaro, Pd. Erasto Kawau. Naibili: Pd. Canut Mitume wa Yesu, Pd. Ngao. Mapadre Makapilano hapa Kituoni: Mt. Yoseph: Pd. Sigisbert, Pd. Leonius, Pd. Rainfrid, Pd. Donat Muller, Pd. Ambros Mosha, Pd. Edwin Hug wote ni Wakapuchin. Waalimu: Sr. Yolanda CDNK. Waalimu Walei: Mr. William Kessy toka Arusha, Mwl. Peter Mutie,Mwl.Denis Kagusha, Mwl. Stevin Kalenzo, Mwl. Philemon Shayo. SHUKRANI
Kwanza tunamshukuru MUNGU BABA, MUNGU MWANA NA MUNGU ROHO MTAKATIFU kutuongoza tangu Chuo chetu kianzishwe hadi sasa tunapoadhimisha Jubilei ya miaka 25 pamoja na mahafali ya 25 ya chuo chetu. Sifa na utukufu ni kwake aliyetuwezesha kufikia hatua hii muhimu. Shukrani kwa padre Fridolin Portman, Mhashamu baba askofu Amedeus Msarikie, askofu Isaac Amani na askofu Ludovic Joseph Minde kwa kushirikiana nasi. Shukrani za pekee ziwaendee wahudumu wa shirika letuSr. Immaculata Haas, Sr. Catherine Mboya, Sr. Dona Marandu, Sr. Christiana Njau na Sr. Margreth Moshi kwa kushirikiana vizuri na Uongozi wa jimbo kuendeleza Utume huu. Tunawashukuru sana wafadhili wetu wote waliotusaidia kwa hali na mali katika ujenzi wa Chuo Chetu. Tunamshukuru Mungu kwa Makatekista wote waliokwisha pita hapa kwa mchango wao na kwa kazi nzuri wanayoifanya kutangaza Injili huko waliko.Tunawashukuru mapadre, watawa na walei wanaotoa huduma katika Chuo chetu Mungu awabariki .Tuanawashukuru Maparoko wote, Wakuu wa mashirika waliowahi kutuma na wanaoendelea kutuma makatekista wao kwa ajili ya kupata Elimu ya Katekesi hapa kwetu.Kwa namna ya pekee tunamshukuru Padre Erasto Kawau kwa ushirikiano mzuri na huduma ya kiroho tunazopokea toka kwake . Shukrani za dhati zimwendee padre Edwin Hug kwa huduma ya kiroho ya kila siku kwa Jumuiya Emmaus. Tunawashuru wahudumu wote wa kituo cha Afya, wafanyakazi wote, majirani, Makatekista wanaohitimu, wanaobaki na watakaokuja kuja kujiunga na Chuo na wote waliojumuika nasi kwa siku hii ya leo. Tunahitimisha historia hii kwa zab. 138:1 Nitakushukuru kwa moyo wote, mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
What we do? See Our Works
We are Real. Meet the Team

SR. MAGRETH MUSHI
Mother superior

SR. ADELA MASSAWE
Vise Mother Superior

SR. IRIMINA F. SHIRIMA
The Congregation Councillor

SR. CATHERIN W. MBOYA
The Congregation Councillor

SR. EMMANUELA B. LORRY
The Congregation Councillor/Mama Nyumba

SR. MARISELA C. SILAYO
Msaidizi wa Mama Nyumba

SR. ALPHONCINA A. SHAO
Dr. Incharge
(Mganga Mfawidhi)

SR. ELIONORA E. KIMARO
Vice Dr. Incharge (Msaidizi, Mganga Mfawidhi)

SR. PAULINE E. URIO
Mkuu wa chuo

SR. APOLINA P. MASSENGE
Makamu Mkuu wa chuo

SR. VERONA E. SWAI
Msimamizi wa mradi wa farm
